MWANDISHI WA KAUNTI.
Mahakama kuu ya Mombasa imetupilia mbali kesi iliowasilishwa na mmoja wa wapiga kura kutoka kwale kupinga uchaguzi wa Gavana wa Kwale Salim Mvurya.
Jaji Mugure Thande amefutilia mbali kesi hio iliowasilishwa na Mwamlole Tchappu Mbwana kwa misingi kuwa naibu gavana wa Mvurya Fatma Achani hakujumuishwa kwenye kesi hio
Wakili wa mlalamishi hatahivyo ameapa kukata rufaa kufuatia uamuzi huo akisema kuwa Jaji Thande hakutumia kipengele chochote cha sheria katika kuitupilia mbali kesi hiyo akisema kwamba Fatuma Achani alichaguliwa na Mvury na wala sio wananchi.
Mbali na kutojumuishwa na naibu gavana huyo mahakama pia imetoa sababu yakuwa stakabadhi za kesi hazikuonyesha tarehe ambapo matokeo hayo yalitangazwa rasmi wala Salim Mvurya kutangazwa mshindi kama gavana wa Kwale.
Hiyo ilivyoendeshwa na uamuzi huo kutolewa katika kipindi cha siku tatu zijazo ili akate rufaa katika kipindi cha siku 14 zijazo.
Jaji mugure Thande amemuamuru Mbwana kulipa kima cha shilingi milioni 2.5 kama gharama ya kesi hiyo.