KAHABA AKIRI KUMWIBIA MTEJA WAKE KUJILIPA HUDUMA ZA URODA.

0
2118

MWANDISHI SAM ALFAN.

Lilian Nyokoa Ngota alihukumiwa kifungo cha masaa matano baada ya kukubali shtaka la kuiba simu yenye thamani ya shilling elfu kumi pesa taslimu.
Hakimu mkuu katika mahakama ya Nairobi Francis Andayi hakuficha mshangao aliopata kwa kumsikia Lilian Nyokoa aliyedai kuwa  kahaba akikiri kimaso maso kwamba alimwibia mteja wake simu aina ya Huawei kujilipa huduna alizotoa.
Mshtakiwa huyo Lilian Nyokoa Ngota hakuficha kazi anayofanya jijini Nairobi. Alisema kwamba  alikuwa  katika harakati za kutafuta chakula chake na watoto wake wakati alipokutana na Joseph Gitonga Mwenda saa kumi na moja alfajiri akiwa mlevi.
walizugumza na wakapatana kwamba angempa huduma za kimapenzi kwa bei walliyokubaliana. Hata hivyo  hakusema kiwango cha pesa, Na alipomaliza haja yake mlalamishi alidai kwamba hana pesa ndipo alipoichukua simu yake
Aliendelea kusema kuwa  hangelienda nyumbani mikono tupu na watoto wanahitaji chakula.
Nyokoa mwenye umri wa miaka 37 alikiri  mbele Andayi kwamba alimwibia Mwenda simu aina ya Huawei katika kilabu maarufu kwa jina Rekemarie ( maana yake wacha waseme)  kilichoko eneo la River Road katika jiji kuu la Kenya.
Ijapokuwa hakimu alishangaa alisema mshtakiwa alivunja sheria.
Alihukumiwa kifungo cha masaa matano kufanyakazi hapa kortini hadi saa tano.
Alikataa alimwibia mwanaume huyo shilling elfu 42,000 kama alivyosema kiongozi wa mashtaka.
Akitoa maelezo mahakama ilielezewa kwamba mlalamishi aliingia katika kilabu kimoja kijulikanacho kwa jina Bettyz na kubugia bia kadhaa.
Korti iliambiwa mlalamishi alijipata katika chumba cha kulala katika hoteli ya Rekemarie bila simu na Shillingi 42,000.
Alipiga ripoti kwa polisi na simu yake ikapatikana na mshtakiwa katika mtaa wa Zimmerman.
Mshtakiwa alipewa siku 14 kukata rufaa. Alitumika kifungo kwa kufagia na kuosha seli katika mahakama kuuu Milimani Jijini Nairobi.
Please follow and like us:

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here